Kampuni ya Facebook ambayo inamiliki pia Mtandao wa Instagram imetoa taarifa kwamba imesitisha kwa muda mpango wa kutengeneza Instagram version maalumu kwa ajili ya Watoto wenye umri chini ya miaka 13 kufuatia Wazazi na Wanaharakati kusema Instagram zitawaharibu Watoto.
Mkuu wa Instagram Adam Mosseri amesema mpango wao umeeleeweka vibaya na kusema hawakuwa na lengo la kuja na Instagram kama wanazotumia Watu wazima ila walipanga kuitambulisha Instagram ambayo ingewapa mafundisho Watoto na kuwapa elimu za masuala mbalimbali yasiyokiuka maadili.
“Wote tunajua Watoto wadogo wanamiliki simu Duniani kote na wanapakua Application zenye mambo ya kikubwa sisi tulipanga kuwaletea Application inayoendana na umri wao ambayo pia Wazazi wangekuwa na uwezo wa kuwafuatilia”
“Kwakuwa Watu wamekosoa na kuja juu tunasimamisha kwa muda mpango huu lakini tutakutana na Wazazi, Watunga Sheria, Watunga Sera na Wadau mbalimbali ili tuwaelimishe zaidi kuhusu hili”