Spika wa Bunge, Dr. Tulia Ackson amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba kwenda kupitia upya swali la Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina na kulijibu tena baada ya kutolewa kwa majibu ambayo amesema yamejibiwa tofauti na swali lililoulizwa na endapo swali hilo halina majibu waje waseme hakuna majibu.
Mpina katika swali lake alitaka kujua ni nini kinachosababisha kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani ya shilingi Trilioni 360 na USD Milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa.