Mnamo Desemba 11, 2022 Mpoto Theatre waliondoka nchini Tanzania kuelekea katika Tamasha kubwa ambalo litafanyika nchini India.
Sasa leo Desemba 14, 2022 Mpoto Theatre tayari wamefika nchini Ethiopia kwaajili ya kuungana na wasanii na wadau wanaoelekea india kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya aliyekuwa Rais Pramukh Swami Maharaj.
Akizungumza kiongozi wa Mpoto Theatre baada ya kufika nchini Ethiopia alisema… “Mpoto Theatre tumefika salama Nchini Ethiopia kujiandaa kuelekea na safari nchini India tukiwa wakilishi pekee ambapo tutakuwa nchini India takribani siku 40 katika tamasha la kihistoria katika kuadhimisha miaka 100 ya Pramukh Swami Maharaj tunategemea kufaniisha safari yetu vizuri na Tamasha litakuwa la kihistoria”