Mbali na kwamba Waandaaji wa African Muzik Magazine Awards ‘AFRIMMA’ kutangaza list ya wasanii watakaowania tuzo zao ambazo hujumuisha Mastaa mbalimbali katika tasnia ya muziki wa Afrika.
Sasa Miongoni mwa watanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo ni Mrisho Mpoto ambae ametajwa katika kuwania tuzo katika kipengele cha Msanii Bora wa Nyimbo za Asili 2022.
Mrisho Mpoto akizungumza na Millardayo.com & Ayo TV alisema.. ‘Kwanza nashukuru Mungu kwa kutajwa katika tuzo hizi kubwa kilichobaki nawaomba Mashabiki na watanzania kwa ujumla nguvu zetu tuwekeze katika upigaji kura nina imani tuzo hii lazima itue Tanzania Ingia katika Website ya Afrimma bonyeza HAPA
“Utakapobonyeza hiyo link basi tafuta kipengele cha Best Traditional Artiste 2022 kuna majina mbalimbali pale pia mtanzania mwenzangu yupo pale Sholo Mwamba tuoneshee utanzania kwanza naimaini hii tuzo itatua Tanzania”- Mrisho Mpoto
Kwenye kipengele alichotajwa Mrisho Mpoto anachuana na wakali akiwemo Mwimbaji wa nyimbo za Singeli Sholo Mwamba, KCEE kutoka Nigeria, Niitettey Tetteh kutoka Ghana, Betty G kutoka Ethiopia, Oumou Sangare kutoka Mali, Manamba Kante kutoka Guinea na Thokozani Langa kutoka Afrika Kusini
Na miongoni mwa wasanii wengine wanaowania tuzo hizo katika vipengele tofauti tofauti ni akiwemo Diamond Platnumz, Maua Sama, Zuchu, Nandy, Jay Melody, Christina Shusho, Barnaba, Sholo Mwamba, Rosa Ree, Hascana, Dj Romy Jons, S2kizzy, Mnenguaji Angel Nyigu.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mwaka huu Mwezi Novemba 19, 2022 nchini Marekani.