Jamii wilayani Geita imetakiwa kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa lika zote huku wakishauriwa kutoa taarifa mara waonapo viashiria hivyo.
Akizungumza katika hafla fupi iliyokuwa imeandaliwa na Shirika la Plan International kwa kushirikiana na Mradi wa KAGSI iliyofanyika katika kata ya nyankumbu kupitia Mchezo wa Mpira wa Miguu uliochezwa katika dimba la Uwanja wa Shule ya Uwanja Diwani wa kata hiyo , John Lunyeba amesema katika kata yake wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto.
” Sisi kama viongozi Serikali ina mpango mzuri tuu wa kuhusu kupambana na ukatili wa watoto upo unaitwa Mtakuwa ko tunazo kamati kwenye Jamii ambazo zinapambana na ukatili wa watoto na akina mama majumbani , “ Diwani Lunyeba.
Diwani Lunyeba amesema amesema toka wameanza na Mkakati huo wa kutokomeza ukatili kwa watoto na akina mama mafanikio yamekuwa makubwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo kuhamasisha pamoja na utaratibu uliowekwa kupitia mikutano ya hadhara ambayo imekuwa ikifanyika bila kusahau vikao vya kata.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa KAGS Kutoka shirika hilo Eliud Mtalemwa amesema wameona ni vyema kuendesha Mradi huo kupitia Mchezo wa Mpira wa Miguu lengo likiwa ni kupunguza na kutokomeza vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto pamoja na kuzungumzia suala la Afya ya uzazi kwa watoto.
“Lengo Michezo ni njia Mojawapo ya kuleta hamasa kwa Jamii na kuwaleta watu pamoja kwenye Jamii na kupeleka ujumbe kwao kwahiyo michezo tunaitumia tuu kama njia ya kufanya hamasa kwa watu kuweza kuja na kuweza kuwafikia ujumbe ambao tumeulenga Kama Mradi, “ Meneja Mradi Mtalemwa.
Bi.Robea Manase ni Afisa kutoka Dawati wa Jinsi Wilaya ya Geita, amesema miongoni Mwa kesi zinazofanywa na Ndugu zimekuwa zikiendelea katika Mashauli mbalimbali kupitia Jeshi la polisi huku wakishirikiana na Maafisa wa Ustawi wa Jamii na kuwapeleka katika Makazi yaliyo salama zaidi.
“Miongoni mwa kesi ambazo zinafanywa na Ndugu ambazo zinakuwa zinaendelea katika Mashauri yetu sisi Jeshi la polisi huwa kesi hizo tunazifikisha sehemu husika ina maana kesi hizo lazima zilipotiwe zifanyiwe utaratibu kwa kushirikiana na Maafisa ustawi kwa hiyo wale wahanga ina maana kama anakuwa sehemu ya kuishi hana tunawachukua na kuwapeleka sehemu salama, “ Afisa Dawati la Jinsia (w) Geita.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita, Bi .Prisca Rupia ameyapongeza Mashirikia yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa Mstari wa Mbele katika kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto huku yakishirikiana na Serikali huku akisema kwenye Jamii kumekuwa na Matukio mengi ya ukatili yakihusishwa na sababu kipato pamoja na tabia za watu.