Top Stories

Kwa mara ya kwanza Saudi Arabia kuzindua jumba la sinema

on

Mambo mengi yanaendelea kuzaliwa na mengine kufufuliwa Saudi Arabia katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na wanawake kuruhusiwa kutazama mechi za mpira live, wanawake kuruhusiwa kuendesha magari, na mengineyo.

Jingine ni hili ambapo serikali ya nchi hii imetangaza kuzindua jumba la sinema kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 35, mnamo April 18, 2018.

Katika kufungua jumba hilo, inaelezwa kuwa sinema ya kwanza kuoneshwa itakuwa Black Panther.

Hii inaelezwa kuwa sehemu ya mpango mkubwa wa kuzindua majumba mengine ya sinema 40 katika miji mbalimbali nchini humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

“Polisi wamempiga kijana risasi ya kisogoni” –Mbunge Maftaha

 

Soma na hizi

Tupia Comments