Top Stories

Msomi wa Degree anayeishi kwa kupiga Gita Coco Beach,nyimbo moja elfu 3,000(+video)

on

Maisha ni safari, Dickson Kambutu ni msomi wa Degree ya Sanaa na Elimu, lakini kwa sasa ni mpiga Gita katika Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam akiwa ni muimbaji wa nyimbo za wasanii wengine na za kwake.

Katika Exclusive na Ayo Tv na millardayo.com Kambutu anasema maisha yake kwa sasa yapo katika ufukwe huo ambapo anajiingizia kipato kisichopungua 30,000 kulingana na msimu husika ambapo anawaimbia watu nyimbo za wasanii wengine na za kwake kwa kiasi cha Shilingi Elfu tatu kwa nyimbo moja.

Historia yake imeanzia mkoani Morogoro akiwa ni mzaliwa wa huko, miaka kadhaa iliyopita aliachana na ajira ya serikali ya Ualimu kutokana na changamoto alizokutana nazo shuleni na kujikuta anakimbilia Dar es Salaam na kuwa Mmachinga wa kuimba muziki maeneo ya Coco Beach.

KAULI YA DC JOKATE KUHUSU SHULE YA KWANZA YENYE BWENI KISARAWE

Soma na hizi

Tupia Comments