Habari za Mastaa

Alichoandika Ray Kigosi kuhusu Chuchu “Tumlete dada yake Jaden’

on

Ikiwa leo September 11 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwigizaji Chuchu Hansy, mzazi mwenzake Ray Kigosi ameitumia siku hii kwa kumuandikia ujumbe kupitia mtandao wake wa Instagram wa kumuomba kuongeza mtoto mwingine wakike.

Ray Kigosi na Chuchu wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda sasa na mapaka sasa wamejaaliwa kuwa na mtoto mmoja wa kiume waliyemuita Jaden. Ray ameandika…>>>“Daaah Sina maneno mengi ya kuandika maana nishaandika mengi sana juu yako hakuna asiyejua nachokuombea Kwa Mungu Wangu wa haki akupe Maisha marefu yenye baraka tele na Mungu ikimpendeza basi tukalete Kadada kake @jadenthegreatest maana Jaden amekuwa mpweke sana au mnasemaje wadau si ni kweli au?….Happy Birthday My Love Mzungu enjoy your Day. @chuchuhansy@chuchuhansy@jadenthegreatest” – Ray Kigosi

 

VIDEO: KUELEKEA UCHAGUZI KINONDONI WASANII WA UZALENDO WAZUNGUMZA

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments