Mwimbaji maarufu, Oluwatosin Oluwole Ajibade, almaarufu Mr Eazi, ametishia kumshtaki mtayarishaji wa nyimbo kwa madai ya kukiuka kandarasi yake.
Kulingana na mwimbaji huyo, alimlipa mtayarishaji huyo ambaye jina lake halikutajwa alimtumia $5,000 kutengeneza wimbo uliokusudiwa kuwa kwenye albamu yake ya kwanza iliyotoka hivi majuzi, ‘The Evil Genius’, lakini hakutuma wimbo huo.
Mr Eazi alisema hatajali kutumia $100,000 kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtayarishaji huyo siku “atakapochoshwa.”
Kwenye akaunti yake ya X, aliandika, “Kuna producer nilimlipa $5000 kutengeneza wimbo ambao ulitakiwa uwe kwenye album yangu na hakuwahi kutuma kazi yangu lol natumai kuwa 5k ilibadilisha maisha yake #TheEvilGenius lakini ipo siku nitakapochoka kukumbuka hilo nitatumia 100k kushtaki ur a*s.”