Habari ya Asubuhi na karibu kwenye matangazo yetu hii leo Alhamisi 17.8.2023
Wakala wa barabara nchini-TANROADS imeendelea na hatua za kwanza za utekelezaji wa wa kujenga barabara itakayounganisha mikoa ya Tanga, Manyara hadi Singida kupitia Handeni – Kiberashi – Kijingu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalaibicha – Chambolo – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida 389 km inayojengwa kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC +F ambayo ni dhana inayompa majukumu mkadarasi ya kufanya usanifu wa mradi, ununuzi wa vifaa, ununuzi wa makandarlsi wengine wa mradi.
Katika hatua hizi za mwanzo TANROADS kama msimamizi wa mradi huu tayari imeshafanya ukaguzi wa barabara itakayounganisha mikoa hiyo mitatu ili kutathmini utekelezaji wa mradi huo ambapo vitawekwa vituo vikuu vinne katika mikoa hiyo ambavyo vimegawanywa kutokana na upatikanaji wa malighafi zitakazotumika katika ujenzi wa Barabara pia kuwashirikisha wananchi waufahamu mradi ili wawe walinzi wa kwanza ili kuepuka kuharibiwa kwa miundombinu.
Aidha, Wananchi wa maeneo ambayo mradi huu utapita hawakuwa nyuma kuonyesha furaha yao ni kwa jinsi gani watanufaika na barabara hihi itakayojengwa kwa kiwango cha lami, akiongea na MillardAyo.com ndugu Musa Rajabu ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji cha Unyaghumpi ameweka wazi changamoto zinazowakumba na ambazo zitatuliwa baada ya mradi huo kukamilika
“Hii Barbara ni changamoto kwa sababu magari yanapita lakini kwa sida na huchangia kuharibika kwa vtyombo vya usafiri lakini pia kufikia mahitaji ya msingi kama hospitali kwa mama wajawazito wakati wa kujifungua imekuwa ni changamoto na kusababisha wajawazito kujifungua wakiwa safarini kuelekea hospitali” alisema Musa Rajabu
Ikumbukwe kuwa changomoto za usafirishaji wa mazao ya biashara yakiwemo pamba pamoja na yale ya chakula Pia ufikiwaji wa huduma za kijamii zote kwa pamoja zinaenda kurahisihwa baada ya ukamilifu wa mradi huu ambar uzo chini ya utaratibu wa EPC+F ambar unauinifaissha serikali moja kwa moja kwa kuisaidia serikali kupata fedha za utekelezaji wa mradi kwa mkupuo lakini pia kuiondoloea serikali kukumu la usanifu wa iradi hivyo kuharakisha utekelezaji wa mradi kwa wakati hivyo kuondoa changamoto za usafarishaji kwa baraka baada ya kukamilika kwa mradi huu