Viongozi wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), wamesema mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), una manufaa zaidi kwa Taifa sio tu kuzalisha nishati hiyo bali utaibua fursa za kiuchumi katika sekta za utalii, kilimo na mifugo.
Hayo yalisemwa na muasisi wa Baraza la umoja wa makanisa ya kipentekoste Tanzania na mkuu wa huduma ya wapo mission international Askofu Sylvester Gamanywa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Mara baada ya Slyvester Gamanywa Mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mradi huo akianbatana na akiambatana na viongozi wenzake.
Gamanywa amewahakishia Watanzania, kuwa mradi wa JNHPP ni salama kwa maendeleo ya Taifa, akisema yeye na viongozi wenzake wametembelea maeneo muhimu ya mradi huo na kujionea shughuli zilizokamilika na kuendelea kufanyika.
“Nawahakikishia wananchi kama yalikuwapo majungu kuhusu mradi basi niwaambia CPCT imejiridhisha kuwa mradi ni salama na una faida kubwa kwa Watanzania na uchumi wa Taifa. Nichukue fursa hii kuwaambia Watanzania kwamba mradi huu ukikamilika Tanzania itaandika historia nyingine,” amesema Gamanywa.
“CPCT tulikuwa tunasikia tu, kuhusu mradi huu, lakini leo tumejiona, kazi kubwa imefanyika katika umalizaji wa mradi ulioanzishwa na Serikali ya awamu ya tano. Ukitembelea mradi huu utajionea mambo mengi, tuishukuru Serikali na wizara kuweka utaratibu wa viongozi wa dini kuja,” amesema Gamanywa.
Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa CPCT, askofu Daniel Awet ameishauri Serikali kuweka utaratibu wa kufanya ukarabati wa mitambo ya mradi huo, pindi utakapoanza kutoa huduma za uzalishaji wa umeme ili kuwepo na tija zaidi.
Amefafanua kuwa mradi wa JNHPP umetumia fedha nyingi, endapo hautakarabatiwa kama ilivyopangwa itakuwa hasara kwa Taifa itakayosababisha shughuli kusimama.Pia ameiomba Serikali kutumia wataalamu wazawa katika kuhakikisha wanautunza mradi huo.
“CPCT tumetembelea na kujionea maendeleo ya mradi huu, tutakwenda kuwaeleza waumini kuhusu umuhimu wake, Lakini tunaomba Serikali itoea elimu inapoanzisha mradi maana wapinzi hawakosi.
Amesisitiza kuwa JNHPP ni mradi mkubwa wa kitaifa wenye manufaa makubwa kwa maendeleo ya Taifa, huku akiipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati, kwa usimamizi bora hadi hatua iliyofikiwa ya asilimia takribani 90.
Kwa upande wao mchungaji wa kanisa la waadventista wa sabato mch. Amon Sikazwe na Askofu Flora Joseph Kaguo kutoka CPCT Taifa Wamesema wanaishukiru Tanzania kwa maendeleo inayopiga hususani kwenye miradi Kama hii ambayo utekelezaji wake uko kwenye hatua za kuridhisha sana
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema moja ya faida za mradi huo ni pamoja na ujenzi wa daraja jingine kubwa katika Mto Rufiji ambalo limeshakamilika, akisema kwa siku zijazo wananchi wanaotoka mikoa ya kusini kwenda Dodoma hawatalazimika kupitia Dar es Salaam badala yake watakatiza katika mradi huo hadi Chalinze.
“Mradi huu una faida katika sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara itakayoanzia maeneo Utete mkoani Pwani ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mikoa ya kusini na Pwani. Pia mradi wa JNHPP utakuwa manufaa kwa sekta za maji kwa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi,” amesema Waziri Makamba.
Pia, Waziri Makamba amesema pamoja na JNHPP, Serikali pia inatekeleza miradi mingie ya kufua umeme ukiwamo wa Rusumo unaojumuisha mataifa ya Tanzania, Rwanda na Burundi ambao ujenzi wake upo mbioni kukamilika.