Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekagua mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ambao DAWASA imepewa jukumu ka kulaza mabomba ya usambazaji.
Bodi imeeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo utakaohudumia wananchi wapatao 438,931 katika Wilaya za Same, Mwanga na Korogwe.