Licha ya serikali na wadau wa mazingira kuendelea kutoa elimu ya utunzaji na uvunaji halali wa Mazao ha misitu bado baadhi ya watu wamekua wakiendelea kufanya Uharibifu Kwa kukata miti hovyo ambapo Takwimu zinazonyesha zaidi ya hekta Laki nne za misitu huaribiwa nchini kila.mwaka
Kutoka na Changamoto hiyo Serikali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la HELVETAS imefanya uzinduzi wa mradi wa Uwezeshaji jamii katika usimamizi endelevu wa misitu (USEMINI) ambapo utasaidia kutunza mazingira kwa kurudisha uoto wa asili na kusaidia kupunguza hewa ukaa.
Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima kwenye uzinduzi wa mradi huo ulihusisha viongozi mbalimbali wa kiserikali na sekta binafsi lengo na kushirikiana katika kutunza mazingira na hivyo kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Malima amesema Mkoa Morogoro katika kuendelea kupambana na Changamoto hiyo imenaza kutekeleza kilimo.cha Miti Miti ya Viungo ikiwemo miti ya karafuu, kakao, michikichi, kahawa na parachichi ambayo pamoja na kuwa miti hiyo ni rafiki kwa mazingira, watu na maji bado itawasaidia wananchi kuongeza kipato chao.
Rc Malima amesema kupitia mradi huo utasaidia katika kutunza mazingira na kuondoa hewa ukaa pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu upandaji wa kwani Miti Hiyo itakua na faida kwao
“Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kupatiwa elimu juu ya matumizi ya nishati mbadala hasa matumizi ya mkaa na kuachana na matumizi ya kuni ambayo yanasababisha wananchi kukata miti kwa ajili ya kupata nishati hiyo”
Naye Mkurugenzi wa Shirika la HELVETAS Daniel Kalimbiya amesema kwa Mkoa wa Morogoro mradi wa USEMINI unatekelezwa katika Halmashauri 4 ambazo ni Mvomero, Ulanga, Malinyi pamoja na Halmahsauri ya Morogoro DC ambapo utazifikia kaya zaidi ya 2000 zenye wanufaika 10000 kata 20 na vijiji 70 katika Halmashauri hizo.
Hata ivyo Kalimbiya amesema Mradi huo utawajengea uwezo wananchi namna ya kusimamia misitu, namna ya kupanga matumizi bora ya ardhi, namna ya kutumia nishati mbadala, pia mradi huo imekusudia kupanda miche milioni moja ya matunda mbalimbali ili kusaidia kurudisha hali ya kawaida yale maeneo ambayo yameathirika na uharibifu wa mazaingira.