Mix

Kiko hapa kilichoamriwa na na Mahakama ya Kwale kwa watuhumiwa waliotaka Mombasa ijitenge na Kenya

on

An inmate rests his hand on the bars of a prison controlled by the SLA/Mini Minawi in Shangle Tubaya villageKiongozi wa kundi la vuguvugu la Mombasa Republic Council (MRC), Omar Mwamnuadzi ameachiwa kwa dhamana ya shilingi laki 8 za Kenya baada ya kukaa jela kwa zaidi ya miezi miwili na wenzake kumi na mmoja.

Watuhumiwa hao wameachiwa huru na Mahakama ya Kwale baada ya kukaa jela kwa zaidi ya wiki mbili kwa kosa la kufanya mkutano kinyume cha sheria.

Mwamnuadzi na wenzake walikamatwa oktoba15 huko Komabi ambapo walifunguliwa mashtaka kwa kosa la kufanya mkutano kinyume cha sheria ambapo washtakiwa walipinga kutenda kosa hilo.

Baada ya kusomewa mashtaka katika mahakama ya Kwale, washtakiwa walipelekwa gereza la shimo la Tewa, Novemba 3.

Kesi hiyo itasomwa tena Januari 12 mwaka 2015.

MRC

Tupia Comments