Habari za Mastaa

Mrembo aliekataa kushiriki Miss World, imeeleza aligoma kuchoma chanjo

on

Miss Netherlands 2021, Dilay Willemstein ambaye alipaswa kwenda Nchini Puerto Rico December mwaka huu kushiriki shindano la Miss World 2021 amegoma kwenda kwenye Fainali hizo kwasababu moja ya vigezo ni lazima Mshiriki awe amechanjwa chanjo ya corona kitu ambacho hayupo tayari kukifanya kwa sasa.

Dilay mwenye umri wa miaka 21 amesema hakujua kuwa ili uendele kwenye Fainali za Miss World ni lazima uwe umechanja lakini baada ya kuambiwa ameona ni bora asiende hivyo aliyeshika nafasi ya pili kwenye mashindano ndiye atayekwenda Miss Word.

Kupitia Instagram akaunti yake Dilay ambaye licha ya kuwa Mwanamitindo pia nia Dancer na Mwimbaji amesema hayupo tayari kuchanjwa kwa sasa na kusema hata kama hiyo ilikuwa ni sehemu ya kutimiza ndoto zake hajutii uamuzi wake kwa kuwa afya yake ni bora kuliko chochote.

OMMY DIMPOZ ASIMULIA KIBA ALIVYOOKOA MAISHA YAKE “HATA NIKIMFUMANIA NA MKE WANGU NA MSAMEHE”

 

Soma na hizi

Tupia Comments