Habari za Mastaa

Mrembo aliyeshirikishwa kwenye Mama Amina ya Marioo, kuinogesha DAR Maison Club

on

N msanii wa kike kutokea Afrika Kusini,  Bontle Smith ambae Mei 21, 2022  usiku wa leo anatarajiwa kuwaimbia  watanzania wanaoupenda muziki wao unaotikisa kwasasa unaofahamika kama Amapiano.

Mrembo huyo atawaburudisha watanzania wakaofika Maison Club iliyopo Masaki Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mmiliki wa Club hiyo Bw. Amour Shamte alisema lengo sio tu wasanii wakigeni kuja kutoa burudani bali pia kufungua milango kwa wasanii wa ndani kufanya nao Collabo.

‘Kwanza hii si mara ya kwanza kwa Uongozi wetu kuwaleta wasanii wa namna hii kwetu sisi ni muendelezo wa burudani na tumekuwa na huu utamaduni wa siku nyingi tu wa kuwaleta wasanii wakubwa kufanya shows hapa nyumbani Tanzania’- Amour Shamte

 ‘Pia kuna wakati tunatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuchangamkia fursa za collabo’- Amour Shamte

‘Na Leo Mei 21, 2022 tutakuwa na msanii wa kike kutoka Afrika Kusini anaitwa Bontle ambae ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri Afrika Kusini lakini pia ameshafanya collabo na Marioo’- Amour Shamte

“Nisingependa kuelezea mengi ila napenda kuwakaribisha watanzania waje leo Maison washuhudie kile kilichoandaliwa kutoka kwa Bontle Smith’- Amour Shamte

Unaweza ukaitazama hapa Collabo ya Marioo na Mrembo Bontle Smith ambae usiku wa leo atakutana na mashabiki zake Maison Club.

 

 

 

 

Tupia Comments