AyoTV

Baada ya Mbunge wa Kilombero kuhukumiwa miezi 6 jela, sheria inasemaje kuhusu Ubunge wake?

on

Mbunge wa kilombero Peter Lijualikani January 11 2017 amehukumiwa kwenda jela miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilombero mwaka 2015.

AyoTV imemtafuta wakili wa kujitegemea Jebra Kambole kutueleza sheria inasemaje pale ambapo Mbunge anahukumiwa kwenda jela, Ubunge wake unakua kwenye nafasi gani? 

Kambole amesema ‘Ikiwa mtu huyo amehukumiwa katika Mahakama yoyote katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kupewa adhabu kwa muda wa zaidi ya miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote atapoteza nafasi yake ya Ubunge, kwahiyo ni kifungo cha zaidi ya miezi 6 yaani miezi 7 na kuendelea

Kumsikiliza Jebra Kambole zaidi unaweza kubonyeza play hapa chini

VIDEO: Mbunge wa Kilombero alivyohoji mbele ya Waziri Nchemba kwanini hapigiwi saluti? bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments