Nani mbunge halali wa Vunjo? kumbuka baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 James Mbatia alitangazwa mshindi wa jimbo la Vunjo ambalo lilikua chini ya Mrema kipindi kilichopita, baada ya huo ushindi Mrema alifungua kesi Mahakamani baada ya kudai amechezewa mchezo mchafu na yeye ndio alistahili kuwa mshindi.
Kesi ikaendelea mpaka leo April 4 2016 maamuzi mapya kutangazwa kwamba Mahakama kuu kanda ya Moshi imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Agustino Mrema hivyo Mahakama chini ya jaji Lugano Mwandambo imeridhia shauri hilo kuisha na kwamba James Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40.
Mrema hakuonekana Mahakamani leo na aliwakilishwa na Wakili wake January Nkobogo ambapo James Mbatia aliyehudhuria Mahakamani leo alisema yafuatayo >>> ‘siku ya leo tumeandika historia mpya hasa kwa jimbo letu la Vunjo, kwa kuwa ukweli ni msingi wa haki na Wanasheria wetu sita waliokua wananitetea mimi‘
‘Baada ya mlalamikaji Mzee wetu Mrema kufikia hatua ya kutoa ushahidi Mahakamani baada ya ushahidi alioutoa Mahakamani na maswali aliyoulizwa yeye mtu mzima akaona upepo sio mzuri kwa upande wake, alipoliona hilo kiutu uzima baada ya kushauriwa na kuona jasho lililomtoka Mahakamani wiki iliyopita akaona hali inazidi kuwa mbaya upande wake‘
James Mbatia kwenye sentensi nyingine amesema >>> ‘Ndugu Mrema amekubali au kukanusha yale yote aliyoleta Mahakamani na ushahidi wake wote aliosema Mahakamani na malalamiko dhidi yangu, Wanavunjo, dhidi ya taasisi za kidini yooote ameyakanusha kwenye hati ya makubaliano, hilo ndio lilikua la msingi ameyakanusha na amesaini mwenyewe’
‘La pili, Mrema amekubali kuwa James Mbatia ndio mbunge halali aliyechaguliwa jimbo la Vunjo, swala la tatu alilokubali ni kweli tungeweza kumdai gharama kubwa, mimi binafsi nimeingia gharama kubwa ikiwemo ya usafiri toka November 2015 alivyoleta shauri hili Mahakamani, sijamdai gharama kwa upande wangu hata senti moja, nimemsamehe kama kawaida yangu‘ – James Mbatia
Cha kumalizia Mbatia amesema ‘Kuna gharama kubwa ambazo ziliingia upande wa jopo lote la Mawakili na amekubali yeye mimi nilipe asilimia 50 ya gharama za mawakili na yeye alipe 50, kwahiyo Mrema amekubali kulipa Mawakili sehemu tu ya gharama ya MILIONI 40 kwa Mawakili wetu na ni agizo la Mahakama na imeingia Mahakamani, kwa hatua ya kwanza MILIONI 15 Mawakili wetu watazipata kwa sababu zipo Mahakamani tayari aliziweka deposit, May atalipa nyingine 15 na kabla ya June atalipa 10 zilizobaki na asipofanya hivyo ni kifungo’
MSIKILIZE JAMES MBATIA ZAIDI AKIIONGELEA HII BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE