Habari za Mastaa

Ni Headlines za Mr Nice kupata shavu nchini Kenya…..

on

Inawezekana kabisa haujamuona Mr Nice kumiliki zile chart za Top 20 za radio lakini ana good news kutokea Kenya ambapo amekubali kufunguka na kusema kwamba amepata shavu la kusaini kwenye kampuni ya Soko Bay International Limited.

Staa huyo akizungumza kwenye millardayo.com  & Ayo TV kayaongea haya..>>Mimi niko Kenya kwasasa naendelea na kazi yangu ya muziki kama unavyojua kwamba nina album mpya iitwayo KIOO chini ya kampuni inaitwa Soko Bay Limited, hii ni kampuni ya wanigeria ambayo wanafanya kazi hapa Kenya’– Mr Nice

‘Kwahiyo imeona umuhimu wangu na according the history ikapenda kufanya kazi na mimi tukakaa chini tukakubaliana ndio maana ninafanya nao kazi na tayari nimeshaanza kufanya tour katika majimbo mbalimbali kutangaza album yangu mpya ya KIOO ambayo inapokelewa vizuri pamoja na shows kibao ningependa kuwashukuru watanzania na East Africa kwa ujumla ‘– Mr Nice

ULIIKOSA HII YA MR NICE ANAFANY MUZIKI KWA NYODO BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments