AyoTV

VIDEO: Maamuzi ya Waziri Nchemba baada ya kutembelea hii shule

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara yake kutembela kila Kijiji katika kila Kata zilizopo Jimboni mwake kuzungumza na wapiga kura na kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Leo ametembela Kijiji cha Ujungu katika Kata ya Mekente na kukuta ubovu wa miundombinu katika Shule ya Msingi Ujungu katika kijiji hicho huku Walimu wakiishi katika mazingira magumu ambapo aliamua kulibeba jukumu la kuboresha miundombinu akiahidi kulishughulikia mapema iwezekanavyo.

Waziri Nchemba amesema…>>>“Kwa kazi nzuri mnayoifanya naahidi leoleo kwa kushirikiana na marafiki zangu tutatengeneza mkaakti wa kushughulikia ukarabati wa madarasa pamoja na nyumba za walimu, walimu tisa kukaa kwenye nyumba tatu hesabu hii haina uwiano kabisa

Hii ni hatua moja kubwa sana na baada ya miaka 15,20 utaona Mbunge anatoka huku, kwasababu hata kijijini nilipotoka walikuwa wanapaita kijijini hivihivi kwa hiyo nitakarabati darasa kama njia ya kuweka mfano bora” –Waziri Nchemba

Kwenye hii video kuna kila kitu…bonyeza play kutazama!!!

Kitu Waziri Nchemba ameagiza baada ya ajali ya moto wa Mbeya 

Soma na hizi

Tupia Comments