Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Msaada wa pikipiki kwa Polisi kulinda Watalii
Share
Notification Show More
Latest News
Iringa :ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 7
September 27, 2023
Ukraine yawashikilia wanaume 2 wanaotuhumiwa kuisaidia Urusi katika mgomo wa Kiev
September 27, 2023
Nigeria: Polisi wamemkamata mwizi wa simu za mkononi akiwa na simu 890 alizoziiba.
September 27, 2023
Mwanamke aliyeshinda taji la Miss Zimbabwe azua mzozo wa ubaguzi wa rangi
September 27, 2023
Indonesia:Wananchi wapigwa marufuku kununua au kuuza bidhaa kwenye mitandao ikiwemo TikTok
September 27, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Mix > Msaada wa pikipiki kwa Polisi kulinda Watalii
Mix

Msaada wa pikipiki kwa Polisi kulinda Watalii

May 9, 2023
Share
5 Min Read
SHARE

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa (wa pili kushoto) akiwa katika pikipiki zilizokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha kwa ajili ya kusaidia katika doria na kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya Arusha, Felician Mtahengerwa (wa kwanza kulia), na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

Arusha Tarehe 18 Mei 2023 – Serikali imeipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa msaada wa pikipiki 15 kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha ili kuimarisha doria zitakazoongeza usalama kwa watalii wanaokuja nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Utalii na Maliasili, Mohamed Mchengerwa alipopokea pikipiki hizo zenye thamani ya TZS 40 milioni kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia kilichopo jijini hapa.

“Ripoti za Benki Kuu Tanzania (BOT) zinaonyesha sekta ya utalii inaendelea kuimarika baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO-19. Mapato yatokanayo na utalii kwa Machi yalifikia Dola za Marekani bilioni 2.787 ikilinganishwa na dola milioni 885 kipindi kama hicho mwaka 2021. Katika mwezi huo, jumla ya watalii 1,574,630 waliingia nchini,” amesema Mchengerwa na kuongeza huku akipongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Samia katika kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour.

“Kipeeke kabisa naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa msaada huu wa pikipiki 15 ambao Benki yetu ya CRDB imeutoa kwa kituo chetu hichi. Pikipiki hizi zitawawezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Askari watakabiliana haraka na dharula jambo litakalosaidia kuimarisha usalama kwa watalii na kuifanya nchi yetu kuwa kivutio kikubwa hivyo wageni wengi kuja kuitembelea.”

Mwaka 2020, sekta ya utalii ilichangia asilimia 10.6 kwenye pato la taifa ila kiasi hichi kilishuka hadi asilimia 5.7 mwaka 2021 kutokana na athari za UVIKO-19 hivyo kuilazimu Serikali kuchuku ahatua za makusudi kuifufua kwa kufuata taratibu za Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanya matangazo kimataifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe kurekodi filamu ya ‘The Royal Tour.’

Ili kuhakikisha usalama wa watalii wanaokuja nchini, Serikali ilianzisha kitengo maalum cha utalii na diplomasia kwa ajili ya kuwahudumia watalii na wanadiplomasia wanaofika nchini kutalii ama kuwekeza kwa haraka.

Kwa kuwa jiji la Arusha ndio kitovu cha utalii nchini, kituo hicho kimejengwa huko na askari wake walipewa mafunzo ya ziada ndani na nje ya nchi juu ya namna bora ya kuhudumia watalii. Vituo vingine vidogo vimefunguliwa katika wilaya za Arumeru, Karatu, Monduli na Longido.

Akikabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa amani, utulivu na usalama katika maendeleo ya nchi kiuchumi, kijamii na kisiasa hivyo ni jukumu la jamii nzima kushiriki kuuimarisha.

“Pamoja na kuwepo hali ya amani na utulivu nchini, bado baadhi ya matukio ya uhalifu hujitokeza kama vile vile uporaji wanaofanyiwa raia hata watalii wanaokuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini. Ili Jeshi la Polisi litekeleze majukumu yake kwa ufanisi linahitaji vitendea kazi vya kutosha,” amesema Nsekela.

Mkurugenzi huyo amesema wanayo furaha kubwa kukabidhi pikipiki hizo ili kuwasaidia askari kukimbizana na wahalifu wanaowapora watalii au kusafirisha mihadarati hivyo kuharibu sifa njema za jiji hili la kitalii.

“Tunachokifanya sasa hivi ni kusimamia mradi wa utalii salama ambao unahitaji askari kuwapo kila walipo wageni. Pikipiki hizi tunazozipokea zitasaidia kuwafikisha askari kwenye maeneo ambako magari hayawezi kufika kwa urahisi zikiwamo barabara nyembamba. Jeshi la Polisi linaaminimazingira salama ni kivutio cha utalii,” amesema Edith ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu.

Hata hivyo, ameiomba Serikali na wadau wengine wa utalii kuliwezesha jeshi hilo kupata pikipiki nyingine 10 zitakazofanya kata zote 25 za Jiji la Arusha kuwa na pikipiki moja ya doria itakayosaidia utekelezaji wa mradi wa utalii salama.

You Might Also Like

Mkutano wa IAWP New Zealand wafungwa, CP Kaganda awakaribisha Wajumbe Tanzania

EWURA kutokomeza mafuta ya makopo vijijini

Mradi wa Umeme wa Upepo wa Zanzibar wapamba moto

Joe Biden atuma salamu za pole kwa Mfalme wa Morocco

Rais Samia azindua ujenzi wa soko la Kizimkazi

TAGGED: habaridaily
Rama Mwelondo TZA May 9, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 114.
Next Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo May 9, 2023
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Iringa :ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 7
Top Stories September 27, 2023
Ukraine yawashikilia wanaume 2 wanaotuhumiwa kuisaidia Urusi katika mgomo wa Kiev
Top Stories September 27, 2023
Nigeria: Polisi wamemkamata mwizi wa simu za mkononi akiwa na simu 890 alizoziiba.
Top Stories September 27, 2023
Mwanamke aliyeshinda taji la Miss Zimbabwe azua mzozo wa ubaguzi wa rangi
Entertainment September 27, 2023

You Might also Like

Top Stories

Ukraine yawashikilia wanaume 2 wanaotuhumiwa kuisaidia Urusi katika mgomo wa Kiev

September 27, 2023
Top Stories

Indonesia:Wananchi wapigwa marufuku kununua au kuuza bidhaa kwenye mitandao ikiwemo TikTok

September 27, 2023
Top Stories

Ukraine kutumia muda wa ukimya siku ya Jumapili kuwaenzi wanajeshi wake

September 27, 2023
Sports

Ukraine imesema haitacheza katika mashindano ya kandanda yanayohusisha timu za Urusi

September 27, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?