Top Stories

Msako wa DC Sabaya, avamia godown akuta magendo, fedha (+video)

on

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Maafisa kutoka Halmashauri kufanya operesheni maalum iliyopelekea kunaswa kwa shehena (Godown) lililokuwa likitumika kuhifadhi vileo feki na bidhaa zingine zikiwemo shehena za mbolea na saruji bila kuwa na vibali halali.

Msako huo uliofanyika kwa kushtukiza usiku wa manane umemnasa Alex Elibariki Swai na Mkewe wanaofanya biashara hizo bila kulipa kodi, huku stika maalum za TRA zikigundulika baadhi kutokuwa halali na zile halali kuwa katika bidhaa tofauti na zilizoidhinishwa awali na Mamlaka.

Wafanyabiashara hao ambao pia walikutwa na lita nyingi za Diesel kinyume na sheria pamoja na fedha kiasi kikubwa ndani wamekabidhiwa kwa vyombo vya dola huku DC Sabaya akiagiza kulindwa kwa eneo lote hilo hadi Mamlaka husika zitakapomaliza shughuli zake na kubainisha taarifa zote za muhimu kwa ajili ya hatua zaidi.

Soma na hizi

Tupia Comments