Habari za Mastaa

Mambo sita usiyoyafahamu kuhusu wimbo wa Msambinungwa wa Tundaman.

By

on

msambiNi mara chache sana inatokea watu kuelewa maana ya misamiati kadhaa inayotumika sehemu tofauti mfano kwenye mashairi ya nyimbo,nahau au hata misemo kwa mfano mtu akikuuliza nini maana ya Msambinungwa unaweza kosa jibu la haraka haraka,tuitumie nafasi hii kumsikiliza Tunda Man akiuelezea wimbo huu alipoongea na millardayo.com.

Swali la kwanza lilikua ni kujua maana halisi ya Neno Msambinungwa,Tundaman alijibu Msambinungwa ni mtu Fulani hivi asiyeeleweka na hafai katika jamii yaani anaweza kuwa muongo,mtu mbaya mtu mwenye vitendo visivyofaa.

Swali la pili tulitaka kufahamu mpaka sasa wimbo wa Msambinungwa peke yake umemfikisha wapi kwenye hili Tundaman alijibu kwanza anamshukuru Mungu kwa mashabiki wake kwa kuipokea vizur huku akitoa mfano kuwa kuna siku moja hivi alikua anashuka kwenye gari anaenda kwa Maneck akawasikia watoto wanaimba walivyomuona wakaanza kupiga kelele.

Kuhusu jumla ya show alizofanya toka aachie wimbo wa Msambinungwa Tunda anadai amefanya show mbili tu kubwa ya kwanza ilikua ya bungeni na nyingine kwa President’Kikwete’ pale kwenye harusi ya Miraji iliyofanyika Mliman City.

Swali lingine lilikua linahitaji kujua Utofauti kati ya wimbo wa Msambinungwa na nyimbo zake zilizopita kwa hili Tunda alijibu>’Msambinungwa ni usemi ambao nimeuleta kwenye ulimwengu wa muziki maana siku hizi mtaani hata ukizingua kidogo tu unasikia watu wanakuita ‘We Msambinungwa’ usizingue so naona Msambinungwa nimefanya vitu vikubwa sana,ukisikiliza Msambinungwa utagundua’

Kingine ni kuhusu video ya Msambinungwa tunda alijibu>’Video ya Msambinungwa niliambiwa wimbo ni mkubwa so na video inabidi iwe kubwa kwa hiyo nilifikiria maana kuna kampuni niliilipa Kenya nikafikiria kufanya nao lakini nikahisi hawatoiweza wale wakenya nikaona video ya wimbo huu nifanye na Abbykazi,mpaka sasa nishashoot vipande kadhaa nimepanga mwezi wa pili kabla ya Valentine niizindue’

Kwa uchache ufahamu wimbo wa Msambinungwa ulivyokuwa>’Idea ya wimbo huu aliitoa mama yake mzazi na Tundaman na aliomba wimbo huo afanye na Marehemu Dr.Remmy Ongala bahati mbaya Dr.Remmy alifariki,baada ya hapo Tundaman alimtajia wasanii 5 wanaofanya vizuri ndipo mama yake akamwambia afanye na Ally Kiba.

 

 

Tupia Comments