Msanii maarufu Taylor Swift kutoka Marekani ametoa dola milioni 5 kusaidia juhudi za kuwasaidia waathiriwa wa vimbunga Helene na Milton vilivyo tokea na kuleta maafa nchini humo.
Shirika la misaada ya chakula, la Feeding America, lilimshukuru Swift kwa ukarimu wake, likisema, “Tunamshukuru sana… Mchango huu utasaidia jamii kujenga upya na kupona, kwa kuwapa chakula muhimu, maji safi, na mahitaji kwa watu waliokumbwa na dhoruba hizi mbaya.”
Kimbunga Milton kilipiga jimbo la Florida, Marekani, na kuacha nyumba milioni 2 bila umeme, huku mafuriko makubwa yakisababishwa na kimbunga Helene wiki mbili zilizopita, kilichopita maeneo ya kaskazini mwa Florida hadi Georgia na Carolina.
Aidha, Taylor Swift, ambaye anajulikana kwa muziki wake pamoja na mchango wake katika misaada, ametoa msaada mkubwa katika nyakati za maafa.
Itakumbukwa Mwaka 2023, alitoa dola milioni 1 kusaidia waathiriwa wa vimbunga katika jimbo lake la asili, Tennessee, nchini Marekani, Pia, amekuwa akitoa michango kwa benki za chakula kwenye vituo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na msaada mkubwa kwa benki ya chakula ya Cardiff, nchini Uingereza.