Habari za Mastaa

Msanii wa Nigeria Fireboy DML kutua Tanzania?

on

Ni Headlines za Sniper Mantana alieahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kimapinduzi hususani upande wa matamasha yanayofanyika TANZANIA, Sasa leo  Octoba 8, 2020  ameteaser clip ikimuonesha mkali wa Nigeria aitwae Fireboy DML huku ikiwa imeambatana na ujumbe ambao unaoashiria huenda siku zijazo kukawa na habari njema kwa wapenzi wa muziki hapa Tanzania.

PICHANI ndie anahusika kuwaleta wasanii wakubwa mbalimbali aitwae Snipe Mantana

IKUMBUKWE Sniper Mantana ameshawahi kuwaleta wasanii wakubwa kutoa burudani wakiwemo wakina Burna Boy, Omarion, Joe Boy , Kranium , Rotimi , Mr Eazi, Tekno, Kiss Daniel , Banky W , Maleek Berry , Liquid Deep, World,Singah na wengineo

Fireboy DML ni msanii wa Nigeria ambae amesainiwa katika lebo ya YBNL Nation na miongoni mwa hit zilizomweka katika ramani ya muziki na kujulikana ni wimbo wake uitwao Jealous ulioachiwa Youtube mnamo March 25, 2019 na kutazamwa watu zaidi 11,027,600

Kwasasa Staa huyo ameshaingiza sokoni album yake mpya iitwayo Apollo yenye nyimbo zisizopungua 11.

Fireboy DML – Vibration

Fireboy DML Scatter

Fireboy DML  Jealous

Soma na hizi

Tupia Comments