Leo April 16, 2019 Shahidi wa 17 katika kesi ya mauaji ya Mwanafunzi wa Shule ya Scolastica Humphrey Makundi amesema mtuhumiwa Hamis Chacha alikiri kuhusika na mauaji ya Mwanafunzi huyo.
Shahidi huyo Hashim Ali ambaye ni askari ambapo awali alikuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro amesema Mtuhumiwa huyo wakati akiandika maelezo yake alimtaja Mmiliki wa Shule hiyo Edward Shayo pamoja na Mwalimu wa Nidhamu wa Shule hiyo Laban Nabiswa ambao walishirikiana kwa pamoja.
Katika hatua nyingine Shahidi wa 16 katika kesi ya mauaji ya Mwanafunzi wa Shule ya Scolastica Humphrey Makundi ameieleza Mahakama jinsi Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwanafunzi alivyompeleka kwenye Shule ya Scolastica nakuonyesha panga alilolitumia kwa mauaji.
Amesema Mtuhumiwa alilichukua panga katika kibanda alichokuwa akikaa na kumkabidhi Inspecta Tenga na baadaye kurudi na Mtuhumiwa moja kwa moja hadi Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nakumrudisha Mtuhumiwa katika Mahabusu.
Akilionyesha panga hilo wakati wa kutoa ushahidi wake amesema amelitambua panga hilo Mahakamani hapo kwa kuwa lilikuwa butu pamoja nakuwa na mpini mweusi.
Akijibu hoja za upande wa utetezi zilizoulizwa na Wakili Daud Shilatu kuhusu mwenye umiliki wa panga hilo ni nani alijibu shahidi huyo “kwa mujibu wa shahidi alisema ni la kwake”
Mwanafunzi Humphrey Makundi anadaiwa kuuawa Novemba 6/2017 na mwili wake kutupwa mto ghona mita 300 kutoka eneo ilipo Shule ya Scolastica.
MZEE KAJICHINJA NA KISU SHINGONI WAKIGOMBANIA MICHANGO YA HARUSI NA WAKE ZAKE