Habari za Mastaa

Msichana amwaga machozi ndani ya Taxi baada ya Dereva ku-rap

on

Tukio limetokea ndani ya Taxi ya Uber nchini Marekani baada ya Msichana Mrembo mwenye umri wa miaka 20 kuchukua TAXI na kukutana na Gremlin, Dereva ambae pia ni Msanii anae-rap ambae alijitambulisha na kumuomba Msichana huyo ruhusu arap moja ya nyimbo zake kama njia ya kujitangaza.

Machozi yalianza kumtoka Mrembo huyu baada ya Dereva kurap wimbo ambao umeendana kabisa na tukio lililomtokea Msichana huyo la kusalitiwa na Boyfriend wake siku chache zilizopita.

Kwenye dakika ya nne Msichana huyo alivua miwani na kuomba kuongea jambo, ndipo alipofunguka kwamba Jamaa alicho-rap ni kama alikuwepo kwenye tukio lililomtokea wiki mbili na nusu zilizopita la Boyfriend wake kum-cheat kwa kulala na Mwanamke mwingine “Nilifanya kila kitu kwa yule Mwanaume”

Baada ya kufika alipokua akienda Mwanamke huyo aliomba kumkumbatia Dereva Taxi huyo ambapo baada ya kushuka Dereva alisema hakujua afanyaje baada ya Abiria wake kuanza kulia na wala hakuwa na nia ya kumliza. (Credits: Gremlin Youtube)

EXCLUSIVE: VANESSA ALIVYOKUTANA NA ROTIMI “AMENIBADILISHA COMPLETELY, NIMEANZA KUISHI NILIVYOSTAHILI”

JUX: “VANESSA NA TREY SONGZ ILIKUA TOO MUCH” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUITAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments