Top Stories

Rais Magufuli aalika Marais wa nchi tano kuja Tanzania

on

Leo October 4, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi 5 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni Peter Van Acker – Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Elisabeth Jacobsen – Balozi wa Norway hapa nchini, Anders Sjöberg – Balozi wa Sweden hapa nchini, Hamdi Abu Ali – Balozi wa Palestina hapa nchini na Mubarak M. Falen Alsehaijan – Balozi wa Kuwait hapa nchini.

Katika mazungumzo na Rais Magufuli baada ya kukabidhi hati zao za utambulisho, Mabalozi hao wameelezea kufurahishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi hizo na wameahidi kuukuza zaidi hasa katika masuala ya biashara na uwekezaji, teknolojia, utalii na uimarishaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na nchi hizo.

Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha shukrani zake kwa viongozi wakuu wa nchi hizo kwa mchango ambao wametoa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mikopo nafuu ya ujenzi wa miundombinu hasa barabara, umeme, maji, huduma za afya, kilimo na uvuvi.

Rais Magufuli amewaalika viongozi wakuu wa nchi hizo kutembelea Tanzania.

Mzee aliepokea Milioni 20 za Rais Magufuli “2020 mwambieni asihangaike akae tuli”

 

Soma na hizi

Tupia Comments