Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune Jumapili alifungua rasmi Msikiti Mkuu wa Algiers, msikiti mkubwa zaidi barani Afrika.
Pia ni ya tatu kwa ukubwa duniani, baada ya misikiti katika miji mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia.
Msikiti huo mkubwa umejengwa katika eneo la ukubwa wa ekari 70 na unaweza kusaliwa na hadi waumini 120,000 kwa wakati mmoja.
Pia ina mnara mrefu zaidi duniani, ambao ni mnara unaotumiwa kwa adhan- mwito wa Waislamu wa kusali.
Msikiti huo ulijengwa kwa muda wa miaka saba, na uligharimu zaidi ya dola milioni 800.
Unatarajiwa kuandaa maombi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, unaotarajiwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo.
Msikiti huo ulikuwa mradi wa Rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika, ambaye alijiuzulu mnamo 2019 baada ya azma yake ya kuwania muhula wa tano madarakani kusababisha maandamano makubwa.