Michezo

Simba yamsajili Mbrazil Vieira aliewaongoza Neymar, Coutinho na Casemiro

on

Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara Simba SC wamemsajili mchezaji mwingine raia wa Brazil kutoka klabu ya ATK FC ya India kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo ni Fraga Vieira mwenye umri wa miaka 26 ambaye ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji.

Vieira amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Brazil ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 iliyokuwa na wachezaji maarufu kama vile Neymar, Philippe Coutinho na Casemiro.

Huyo ni mchezaji wa pili raia wa Brazil kusajiliwa na Simba katika kipindi hiki cha usajili baada ya wiki moja iliyopita kutangaza usajili wa mshambuliaji Wilker Da Silva.

BAADA YA KIPIGO AMUNIKE KAFUNGUKA”HAKUNA TIMU ILIYOKUJA HAPA KUFUNGWA”

Soma na hizi

Tupia Comments