Michezo

Ukweli wa Simon Msuva kuhusu ile ya kufanya majaribio South Africa.

on

bidvestSimon Msuva ni winga mshambuliaji wa klabu ya Dar Es Salaam Young African ambae msimu uliomalizika aliibuka kuwa mfungaji wa bora wa Ligi Kuu Tanzania bara katika msimu uliomalizika wa mwaka 2014/2015 ambapo awali kulikuwa na taarifa za Simon Msuva kwenda kufanya majaribio pasipo ridhaa ya viongozi wa Yanga.

Msuva alipata nafasi ya kuongea na millardayo.com na kuyasema haya >>> kwa ufupi ilikuwa hivi ile timu ilileta ofa lakini waliileta katika mazingira ambayo Yanga hawakuwa wameridhika waliona  kama imeletwa kihuni sababu haikufika kwa uongozi moja kwa moja ilikuja ila ikawa imefahamika kuwa Simon anatakiwa kwenda katika timu akafanye majaribio  ili yule kocha aweze kunichukua katika timu nikaletewa tiketi

msuva_bid

Simon Msuva akiwa Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio

Kabla sijaondoka siku mbili kabla nikawaambia viongozi, wakaniambia huwezi kuondoka kuna mechi mbili ya Azam FC na Ndanda, ila nikawaambia ubingwa tushapata wakagoma wakati mimi nahitajika South kabla ya Ligi haijaisha, hata hivyo nilikwenda kibishi nikakaa siku nne sababu ilikua ni lazima niende ndani ya hiyo time ambapo kocha wa South akanikubali na akaniambia kila kitu tutamaliza ila baadae dau walilokuwa wanataka Yanga na wale wakawa wameshindwana” – Simon Msuva

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments