Shirika la Maendeleo ya Elimu la Africa Academy Limited kupitia mpango wa elimu ya sayansi nchini, limeendesha Kongamano linalohusu kutekelezaji wa mtaala wa elimu ya sayansi kwa vitendo kwa kuhusisha utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendeshwa na wanafunzi nchini.
Mkurugenzi wa Shirika hilo Profesa Nuhu Khabitu amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuunganisha taasisi na wadau mbalimbali wa sekta ya hiyo katika kutekeleza mtaala rasmi wa sayansi kwa vitendo kwa wanafunzi ili kuwasaidia kuwa na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika masuala ya Sayansi na Teknolojia.