Michael Koplandi Rai wa Uingereza mwenye umri wa miaka 39 amekuja Tanzania na kupanda mlima Kilimanjaro akiwa na friji lake lenye uzito wa kilo 25 baada ya kupanda zaidi ya milima 30 huku lengo lake ikiwa ni kufahamisha ulimwengu wanaume kuachana na msongo wa mawazo unaopelekea wanaume kujiua
Michael anasema ameanzisha kampeni hiyo baada ya kukutana na changamoto ya kumzalisha msichana mwenye umri wa miaka 16 wakati akiwa jeshini nakuamua kuachana na jeshi akiwa na miaka 24 baada ya mke wake wa kupata mtoto wa pili
Ameongeza kuwa ili aweze kufanikisha kampeni hiyo na kuweza kufikia idadi kubwa ya watu aliamua kuja Tanzania kupanda mlima kwa sababu ni mlima ambao hauhitaji kamba wala vyuma kufika,na ndio mlima pekee mrefu zaidi kuliko yote barani Afrika
Mgeni huyo ameanza safari yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro March 18,kwa kupitia njia ya Lemosho akiwa na timu ya waongoza watalii saba wa kampuni ya Ahsante tours na wanatarajia kushuka March 25,2024 na atatumia siku nane mlimani