Mtambo wa mabao Jamie Vardy, kutoka Leicester city atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa kufuatiwa taarifa za madaktari wa timu hiyo kutaka kumfanyia operesheni baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa ngiri.
“Tumekuwa tukimchunguza kwa muda mrefu, ila kwa sasa hawei tena kujizuia bora apatiwe matibabu mapema kuna michezo mingi mbele,” Brendan Rogers kocha wa Leicester city.
Alipoulizwa ni mshambuliaji gani atatumika kama mbadala wa Vardy kati ya Ayonze Perez na Ihenacho, Rogers alijibu “Kipindi cha nyuma tulicheza bila Vardy tukafunga na mchezo tukashinda.”