Habari za Mastaa

Mtangazaji wa Clouds FM apewa shavu na Makamu wa NBA

on

Mtangazaji wa vipindi vya michezo Clouds FM Nicasius Nicholaus maarufu kama Kotinyo amepewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kwanza wa Academy Tanzania inayolenga kusaidia vijana, makocha na viongozi wa michezo kufika mbali na kuongeza maendeleo ya elimu.

Kotinyo amepewa nafasi hiyo na Makamu wa Rais wa NBA, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBA Africa na Rais wa ligi mpya ya Afrika, (Basketball Africa League) Amadou Gallo Fall, ambapo wameamua kuleta Academy ya kwanza ya mpira wa Kikapu Tanzania.

Amadou ameeleza kuwa hii inatokana na jitihada za Nicasius (Kotinyo) kumwomba kwa miaka 2 kuileta Academy inayofahamika kama SEED (Sports For Education and Economic Development) ambayo aliianzisha zaidi miaka 20 iliyopita.

Academy hii ya SEED imezalisha wachezaji wengi akiwemo Gorgui Dieng anayechezea klabu ya Memphis Grizzlies ya NBA.

BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MAKONDA ALIVYOKATA KEKI KWENYE PARTY YAKE.

 

Soma na hizi

Tupia Comments