Jukwaa la Vijana la Umoja Wa Afrika ambalo lipo chini ya Umoja Wa Afrika (AU) limemtangaza Mtanzania Sylivia Mohamed Mkomwa kuwa Mtanzania pekee miongoni mwa Vijana 25 kutoka Nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika katika Kamati ya Vijana Washauri wa Kitengo cha Vijana Umoja wa Afrika @auyouthprogram katika kuchagiza masuala ya ushiriki wa Vijana Afrika na nje ya Afrika.
Jukwaa hilo limesema mchakato wa kumpata Sylivia ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Watu wengine mbalimbali kutoka Mataifa ya Afrika na Ulaya, ambapo walipokea maombi zaidi ya 2000.
Sylivia Mkomwa ni Afisa Miradi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Kijamii ya Global Peace Foundation Tanzania ambaye pia amekua Mdau mkubwa wa masuala ya kijamii hususani Vijana katika ujenzi wa amani.
Sylivia amekua akijitolea katika kazi mbalimbali za kijamii na kushiriki mikutano mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania kuhamasisha ushiriki wa Vijana na ushirikishwaji wa vijana katika mambo mbalimbali hususani katika ujenzi wa amani kwa maendeleo endelevu.