Top Stories

Mama aua watoto wake sita kwa kuwakata mapanga, nae afariki (+video)

on

Watoto sita wameuawa na wanne wamejeruhiwa kwa kucharangwa kwa panga na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nana Maganga (35 )  anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, Mwanamke huyo ambaye anaishi Tabora, naye aliuawa wakati akidhibitiwa na wananchi.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tabora Emmanuel Nley akizungumza juu ya mauaji ya watu hao, amesema Nana kutokana na tatizo lake la ugonjwa wa akili alikwenda kwa mganga wa jadi ambaye ni shemeji yake kwa lengo la kupatiwa matibabu ndipo mkasa huo wa kuwakata kwa panga watoto wake ambao alikuwa amelala nao katika chumba kimoja ulipotokea.
RPC Nley amesema kuwa waliomdhibiti Nana wakati akitekeleza mauaji hayo akiwemo shemeji yake, walidai walimdhibiti kwa kumfunga kamba ambapo baadaye mwenyewe alikunywa sumu na kupoteza maisha, jambo ambalo hata hivyo, kamanda Nley amelikanusha.

MWANAMKE AKUTWA MTUPU KWENYE NYUMBA YA MWANAJESHI, WANANCHI WAFUNGUKA ’’ANAWANGA”

Soma na hizi

Tupia Comments