Mtendaji mkuu wa club ya Man City ya England Ferran Soriano ameweka wazi na kufunguka kuwa mpango wa UEFA kuifungia Man City kushiriki michuano yoyote ya Ulaya inayoandaliwa na UEFA kwa kudaiwa kukiuka sheria ya matumizi (Financial Fair play) imekaa kisiasa zaidi kuliko haki.
“Mashabiki nawahakikishia vitu viwili kwamba cha kwanza kabisa tuhuma hizo ni uongo cha pili ni kwamba tutafanya kila kitu kinachowea kuthibitisha kuwa tuhuma hizo sio za kweli, kitu muhimu ninachotaka kusema leo tuhuma sio za kweli”>>>Soriano
Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia tovuti ya Man City Ferran ameeleza kwa kina ili kuwatoa hofu mashabiki wakiwa mbioni kukata rufaa, UEFA iliifungia misimu miwili Man City (2020/21&2021/22), sheria waliyovunja Man City (FFP) inaeleza kuwa hairuhusiwi club kufanya matumizi ya juu zaidi kuliko kiasi inachoingiza.
VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA