Top Stories

Trump ameshtakiwa Mahakamani na Dereva wake kabla hajawa Rais

on

Leo July 11, 2018 Noel Cintron ambaye alikuwa dereva wa Donlad Trump amemfungulia shtaka bosi wake kwa madai ya kutaka kuongezwa mshahara pamoja na malupulupu mengi yakiwemo kulipwa kwa kazi alizokuwa akizifanya katika muda wa ziada na mengine hii ni kutokana na kumfanyia kazi kwa zaidi ya miaka 20 hadi alipoingia Ikulu mwaka 2016.

Katika shtaka lililofunguliwa na Noel amesema alikuwa akilipwa Dola $62,700 kwa mwaka na mnamo 2008 alilipwa Dola 68,000, na akapata nyongeza nyingine mwaka 2010 ambapo Trump hakumwongeza tena.

Ameongeza kwamba pamoja na mshahara huo kufikia Dola 75,000 kwa ongezeko la kawaida,  alilazimishwa kulipia gharama za afya za kampuni la Trump Corporation ambazo zilifikia Dola 18,000 kwa mwaka.

Anadai pia amefanya kazi za ziada kwa muda wa saa 3,300 mnamo miaka sita iliyopita, na hivyo kwa mahesabu hayo anadai kulipwa kiasi cha Dola 178,000.

“Afadhali ulime Bangi kuliko Kahawa” wananchi wamemwambia Prof. Tibaijuka

 

Soma na hizi

Tupia Comments