Felister Danda anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 – 23 mkazi wa mjini Njombe amekutwa ameuawa kwenye eneo la msitu wa miti ya kupandwa ya TANWAT huku karibu ya mwili wake uliokuwa na damu akiwepo mtoto wake Ivan Mbise anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili.
Ayo TV imefika nyumbani kwa Lusimiko Mwenga katika eneo la Igeleke mtaa wa Kambarage alikokuwa anaishi Felister wakati anatafuta maisha ambapo amesema amefika katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Kibena na kuutambua mwili wa shemeji yake.
“Felister ni shemeji yangu nilikuwa nakaa naye hapa Igeleke kwa muda ambao alikuwa anatafuta maisha baada ya hapo akaenda kuolewa na baada ya muda kidogo alihitilafiana na bwana ake akaenda kutafuta maisha mwenyewe kwa kupanga chumba huku tukionana na kupigiana simu tukiendelea na maisha lakini siku ya jana watu ambao wanakaa mtaa mmoja wakaja kuniambia nikaenda dukani kwangu nikaangalia picha zinazotembea mtanadaoni nikaona ni mtoto wa shemeji yangu”alisema Mwenga