Polisi Mkoani Dodoma wamesema mnamo November 20,2021 katika Kijiji cha Mkoka Wilaya ya Kongwa, Dodoma, Mtoto wa Kiume mwenye miaka minne, Mwanafunzi wa Chekechea alilawitiwa na Mwanaume mwenye umri wa miaka 16.
Mtuhumiwa ambaye ni Ndugu wa Mtoto huyo na wanaishi nyumba moja alimwingilia kinyume na maumbile wakati Wazazi wa Mtoto wakiwa hawapo nyumbani, Mtuhumiwa amekamatwa na hatua za kisheria zinachukiwa dhidi yake.
“Wazazi wachukue tahadhari sana, hawa Wageni pamoja ya kuwa ni Ndugu zao lakini wachukue tahadhari sana kuwaacha walale na watoto wao” ——— Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga