Mtoto wa miaka 14 wa Navakholo, Kaunti ya Kakamega amemuua mwanafunzi mwenzake wa miaka 10 kwa kumpiga na kitu kichwani na kuutupa mwili wake Mto Simakina baada ya kugundua kuwa amekula ugali wake.
Inaelezwa kuwa, Mtoto huyo aliporudi Shule aliambiwa kuwa Jirani yao huyo ameshakula Ugali Kunde aliowekewa, ndipo alipomfuata machungani na kumshambulia.
OCPD wa Navakholo, Richard Omanga amesema mwili wa mtoto unafanyiwa uchunguzi zaidi na Polisi wanamshikilia mtuhumiwa huyu kwa mahojiano zaidi.