Top Stories

Mtoto apiga simu Polisi wakaangalie midoli yake

on

Polisi nchini New Zealand wamepongezwa kwa upendo wao baada ya kuamua kufika nyumbani kwa Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne ili kuangalia kama midoli yake ni mizuri kama alivyoiambia Polisi kupitia namba za dharura.

Mtoto huyo alipiga namba za dharura za Polisi na baada ya simu kupokelewa na Askari wa Kike akasema ——— “Askari naweza kukuambia kitu?, midoli yangu mizuri unaweza kuja kuiona!?”

Baada ya Polisi wa Kitengo cha Dharura kutoa taarifa kwa Boss wake kuwa hakuna dharura bali Mtoto anataka midoli yake ikatazamwe na Polisi, Boss akatoa taarifa kwa Askari walio karibu na anuani ya ilipopigwa simu waende ——— “kuna Mtoto wa miaka minne anataka Polisi wakaione midoli yake, OVER”

Constable Kurt alifika anapoishi Mtoto huyo na Wazazi wake na akaiona midoli na kupiga nae picha huku akisema Mtoto huyo anafanya vizuri pia darasani ——— “tunawaomba Watoto wasitumie namba ya dharura 111 kuwapigia Polisi waende kwao kutazama midoli lakini tukio hili la Mtoto huyu limetuvutia”

KAMANDA AELEZEA THE CASK BAR KUTEKETEA MWANZA ” UCHUNGUZI WA KINA”

Soma na hizi

Tupia Comments