Mtoto wa mchezaji nguli wa soka David Bekham ,Cruz Beckham amepost picha kwenye page yake ya instagram na kuonesha saa yake mpya ya Rolex yenye thamani ya £32,900 (Mill. 97 )huku akipata glasi yake ya kwanza ya pombe akiwa na baba yake na kaka yake Romeo wakati akisherehekea kutimiza miaka 18 tangu kuzaliwa kwake.
Rolex Submariner saa hii inasemekana kuwa bei ya kuagizwa kwake inaweza kugharimu zaidi ya bei yake ya kununulia , huku tovuti moja ikitoa toleo la zamani la saa kwa si chini ya £48,990 na saa hii ni waterproof na ilikuwa maalum kabisa kwaajili ya wanamaji ( submariners)
Si mara ya kwanza Cruz kupewa zawadi ya saa maarufu nchini Uswizi, ya bei ghali zaidi na wazazi wake
“Heri ya Siku ya Kuzaliwa Cruzie!! Sisi sote tunakupenda sana na tunajivunia kijana mzuri ambaye umekuwa.” Victoria
David pia alishiriki video hiyo na ujumbe: ‘Siku ya kuzaliwa yenye Furaha ya 18 kwa mvulana wetu mzuri zaidi mwenye nguvu za ajabu na moyo mkuu tunajivunia wewe na tunakupenda sana Cruzie’.
Mwaka jana mtoto huyo aliripotiwa kusainiwa na Tap Music, ambaye hapo awali alisimamia kazi za mwanamuziki kama Dua Lipa na majina mengine makubwa ikiwa ni pamoja na Ellie Goulding na Lana