Michezo

Mtoto wa Kolo Toure, Yassine asajiliwa Leicester

on

Klabu ya Leicester City imemsajili mtoto wa mlinzi wa zamani wa Arsenal na Liverpool Kolo Toure, Yassine kwa mkataba wa miaka miwili.

Yassine ambaye tofauti na baba yake yeye anacheza kama winga wa kulia na atakuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha U18 cha Leicester.

Kinda huyo aliyezaliwa wakati Kolo akiichezea Arsenal ana uraia wa Uingereza na Ivory Coast na ana kibali cha kuchagua kuchezea Taifa mojawapo.

Soma na hizi

Tupia Comments