Shamsa Ramadhani ni mtoto wa miaka 9 kwa umri wa mtoto huyu ndie mwenye jukumu la kumuuguza Bibi yake kwa zaidi ya miaka mitatu akimpatia huduma zote ikiwa ni pamoja na kumsafisha Bibi anapopata haja.
Mtoto huyu anasilimua baada ya kifo cha Mama yake hajawahi kumuona tena Baba yake licha ya kuwa yupo hai lakini hiyo haijamfanya Shamsa kupunguza mapenzi kwa Bibi yake na hata wanapoishi wamehifadhiwa kwa muda tu na msamalia mwema.