Mahakama ya kikatiba ya Uganda imemtaka Mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kujibu shtaka analotuhumiwa nalo la kueleza nia yake ya kuwania urais akiwa bado anahudumu katika jeshi la nchi hiyo.
Wakili wa haki za binadamu Gawaya Tegulle aliiomba mahakama katika mji mkuu, Kampala, kumzuia Jenerali Kainerugaba kufanya shughuli za kisiasa akiwa bado anatumikia jeshi.
Gawaya pia anataka jenerali huyo afunguliwe mashtaka ya uhaini kufuatia madai yake ya njama ya kumrithi babake kwa kutumia mbinu haramu, Jenerali Kainerugaba, Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Uganda ana siku 10 kuwasilisha majibu yake.
Mnamo tarehe 2 Mei, alitangaza mipango ya kuzindua mpango wa kisiasa, na kuchochea uvumi kwamba alinuia kumrithi babake wa muda mrefu.
Mnamo Machi 8, alitangaza kustaafu Jeshi kwenye Twitter lakini Rais Museveni alikataa, Rais Museveni amekanusha kumuandaa Mwanae kuchukua wadhifa wake.