Michezo

Mtoto wa Rooney asaini Man United

on

Mshambuliaji wa zamani wa Man United Wayne Rooney kupitia ukurasa wake wa instagram amethibitisha kuwa mwanae Kai (11) amesaini mkataba wa kujiunga na timu za vijana za Man United.

Kai ndio mtoto wa kwanza wa Rooney katika list ya watoto wake wanne wa kiume aliyozaa na mkewe Coleen Rooney.

Rooney (38) ambaye alijiunga na Man United 2004 akitokea Everton kwa sasa ndio kocha wa muda wa timu ya Derby, hadi anaondoka Man United Rooney alikuwa kaifungia jumla ya magoli 253 katika michezo 559 hiyo ni katika kipindi cha miaka 13 alichodumu Man United.

Soma na hizi

Tupia Comments