Jumapili January 19 kulitokea kifo cha kutatanisha cha mtoto aliyekua akisoma shule ya msingi Yombo Vituka darasa la pili ambaye alikua anaingia darasa la tatu mwaka huu Rahma Abeid Karim ambaye taarifa inasemekana alijinyonga chumbani kwake.
Millardayo.com imefatilia kwa undani taarifa hizi baada ya kuzipata kwa sababu ya umri mdogo aliokua nao marehemu na pia tulitaka kufahamu usahihi wa taarifa hizi za kujinyonga ambapo tulipata nafasi ya kuzungumza na baba wa mzazi wa Rahma Mr.Karim Abeid Kihiyo.
Mr.Kihiyo alianza kuelezea siku ya tukio ilivyokua>>’Ni kifo cha kusikitisha nakumbuka siku ya Jumapili[Jan 19] nilikuwa chumbani kwangu,kawaida mwanangu huwa ana tabia ya kuniamsha baba leo huendi kazini nikamwambia mwanangu naenda,tukanywa chai nae’
‘Baada ya hapo nikaenda Kariakoo nilikua na shughuli za Kariakoo,ilipofika saa 6 mchana nilipigiwa simu na mke wangu akiwa analia,akisema mtoto kafa,mtoto kafa nikawa najiuliza nani kafa kwa sababu hakuna mgonjwa nyumbani,nikampigia simu mpangaji wangu akanambia mtoto Rahma ni marehemu sasa hivi’
‘Nilikosa nguvu Kariakoo wenzangu walinichukua kwa gari namimi nilikua na gari yangu kule lakini sikujitambua kama nilikuwa nalo sikumudu kuendesha hivyo wakanileta nyumbani,kutokea kule mbele ya barabara yetu hii ya Kigelagela nikaona watu wamejaa nikajua kweli tukio limetokea’
‘Baada ya kufatilia nikaambiwa mama alikua anafua na mtoto nje,baadaye mama akamwambia mtoto nenda ndani kanichukulie nguo zako za shule nikufulie,mtoto akaingia ndani baada ya muda kidogo mama alianza kumuita,lakini hakuitikiwa akahisi labda mtoto kanyamaza tu’
‘Akaingia ndani aliposhika mlango wa chumbani kwao mlango ulikua umefungwa,akaona azunguke dirishani akamuona mtoto kajiinamia kitandani halafu kajifunika nguo,ikiwa juu kajifunika mtandio chini kajifunika shuka,mama akawa hana wasiwasi pale dirishani aliendelea kuita’
‘Mama alipoona kimya akakimbia ndani akamuita mwanangu mwingine Zena wakapiga ule mlango bahati nzuri ulifunguka kufika akamkuta mtoto yuko hoi kitandani akamchukua akamuweka ‘Sebuleni’ wakati huo alikua anahema kwa mbali sana wakaomba msaada kwa majirani,lakini bahati mbaya hawakuwahi kufika hospitali kwani alifariki wakiwa njiani.
Marehemu Rahma katikati akiwa na ndugu zake
Msikilize Baba mzazi wa marehemu akielezea tukio hili la kusikitisha kwa kubonyeza play.