Shirika la Afya Duniani (WHO) siku ya Jumanne lilisema kuwa mtu mmoja hufa kutokana na kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sita, na zaidi ya theluthi moja ya waathiriwa wote wana umri wa chini ya miaka 20.
“Wakati nyoka wenye sumu husambaa kwa upana katika maeneo ya dunia ya kitropiki na baridi, na hatari kubwa zaidi kwa afya ya umma hutokea katika mataifa ya kipato cha chini na cha kati ‘ David Williams, mtaalamu wa WHO kuhusu nyoka na kuumwa na nyoka, aliambia mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva.
Matamshi yake yalikuja kabla ya Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji kuhusu Kuumwa na Nyoka, ambayo huadhimishwa kila Septemba 19.
Kulingana na mtaalamu huyo, visa milioni 1.8-2.7 vya kuumwa na nyoka hutokea kila mwaka, na hivyo kusababisha vifo kati ya 81,000-138,000.
Wengi wa kuumwa na nyoka hutokea Asia, Afrika, Marekani Kusini, Williams alisema, wakati inakadiriwa watu milioni 1.2 walikufa kutokana na kuumwa na nyoka nchini India pekee mwaka 2000-2019 – wastani wa 58,000 kila mwaka.
Alisisitiza kuwa si kila mtu anayeumwa na nyoka husababisha vifo, lakini kwa kila anayefariki dunia, watatu zaidi hubaki na “ulemavu wa muda mrefu au wa kudumu” mfano kovu la mwili kudhoofika au hata kukatwa viungo.
Akizungumzia tishio hili, alisema maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kuumwa na nyoka hayana uwezo wa kupata matibabu ya kutosha.